Vibali vya Ajira kwa Wageni Ofisi ya Waziri Mkuu - Sera, Bunge, Uratibu, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu imeanzisha Mfumo wa Mtandaoni wa Maombi na Utoaji wa Vibali vya Kazi (OWAIS). Mfumo huu umeunganishwa na Mfumo wa Mtandaoni wa maombi ya Vibali vya Makazi (e-Permit), unaosimamiwa na Idara ya Uhamiaji. Mfumo huu uliounganishwa unawawezesha waombaji kuwasilisha maombi yao ya Vibali vya Kazi/Makazi kwa njia ya kielektroniki, kulipa ada zinazohitajika, kupokea taarifa za maendeleo ya maombi na Notisi ya Idhini mtandaoni kupitia barua pepe zao.
Baadhi ya nyaraka muhimu ni pamoja na:
Mchakato wa Maombi
Ili kufikia Mfumo wa Mtandaoni wa maombi ya Kibali cha Kazi/Makazi, waombaji wanapaswa kutembelea tovuti rasmi ya Ofisi ya Waziri Mkuu: www.kazi.go.tz AU tovuti rasmi ya Idara ya Uhamiaji: www.immigration.go.tz na kubofya kiungo kitakachowawezesha kuanza mchakato wa maombi. Ifuatayo ni mchakato kamili wa maombi:- Mwombaji anatakiwa kujisajili kwenye Mfumo wa Mtandaoni kwa kutumia barua pepe yake au kuunda mpya.
- Kisha atatakiwa kufungua akaunti kwa kujaza majina yake na taarifa za kampuni au taasisi inayotaka kumwajiri.
- Mwombaji atatengeneza nenosiri (password) litakalotumika kuingia kwenye mfumo wakati wowote.
- Atawasilisha taarifa kwa kubofya kitufe cha SUBMIT na akaunti itaundwa.
- Ataingia kwenye mfumo wa OWAIS na kuendelea kujaza fomu ya maombi mtandaoni.
- Baada ya kujaza fomu, atawasilisha kwa kubofya SUBMIT.
Nyaraka Zinazohitajika
Kabla ya kujaza fomu, mwombaji anatakiwa kuandaa nakala zilizothibitishwa (certified copies) za nyaraka zote kwa ajili ya kupakia mtandaoni.Baadhi ya nyaraka muhimu ni pamoja na:
- Barua ya maelezo (Justification Letter)
- Picha ya pasipoti yenye background ya bluu
- Nakala ya pasipoti halali (isiyopungua miezi 6 kabla ya kuisha muda wake)
- Vyeti vya taaluma/ufundi
- CV (Wasifu binafsi)
- Mkataba wa ajira
- Maelezo ya kazi
- Leseni za biashara
- Cheti cha TIN, VAT na Tax Clearance
- Cheti cha usajili wa kampuni/taasisi
- Barua ya utambulisho wa mwajiri
(n.k kulingana na daraja la kibali)
Masharti ya Nyaraka
- Ziwe katika mfumo wa PDF (isipokuwa picha ya pasipoti)
- Zisiwe zaidi ya KB 500
Madaraja ya Vibali vya Kazi
- Daraja A: Wawekezaji au waliojiajiri – USD 1,000
- Daraja B: Wataalamu – USD 500
- Daraja C: Taaluma nyingine – USD 1,000
- Daraja D: Shughuli za kidini/kiutu – USD 500
- Daraja E: Wakimbizi – Bure
Malipo
Mwombaji atapokea Control Number baada ya kuwasilisha maombi, kisha atalipa kupitia benki au mtandaoni (Visa/MasterCard). Mfumo utafikisha maombi kwa Kamishna wa Kazi na baadaye kwa Uhamiaji kwa maamuzi.Mchakato wa Utoaji wa Kibali
Baada ya kulipa ada ya Kibali cha Makazi:- Mwombaji ataitwa kutoa alama za vidole na picha
- Atapewa kadi ya e-Permit yenye taarifa za vibali vyote viwili
Taarifa Muhimu
- Tumia tovuti rasmi pekee kufanya maombi
- Chagua daraja sahihi la kibali
- Soma miongozo kabla ya kujaza fomu
- Lipa kwa kutumia control number husika
- Ada hazirudishwi wala kuhamishwa