Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA), kwa kushirikiana na Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), inatekeleza mradi NBC Wajibika Scholarships kwa ajili ya ufadhili wa mafunzo ya ufundi stadi kwa vijana wa Kitanzania. Katika awamu ya kwanza vijana wa Kitanzania 588 watawezeshwa kupata ujuzi wa vitendo unaokidhi mahitaji ya soko la ajira, kuongeza fursa za ajira na kujiajiri, pamoja na kuchangia maendeleo ya uchumi jumuishi nchini.